Exodus 30:1-4

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

(Kutoka 37:25-28)

1 a“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. 2 bMadhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,
Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.
na kimo cha dhiraa mbili,
Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo.
3 eFunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. 4 fTengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu.
Copyright information for SwhNEN